8. Pambano Kuu
Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika katika pambano kuu baina ya Kristo na Shetani kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake, na utawala wake juu ya ulimwengu. Ugonvi huu ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa uhuru wa kuchagua, katika kujiinua akawa shetani, mpinzani wa Mungu, na kupelekea sehemu ya malaika kwenye uasi. Akaingiza roho ya uasi katika ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu na Hawa kuingia dhambini. Dhambi hii ya mwanadamu ilileta matokeo ya upotoshaji wa sura ya Mungu katika wanadamu, uvurugaji wa ulimwengu ulioumbwa, na mwishowe kuteketea wakati wa gharika iliyoukumba ulimwengu wote. Ukitazamwa na viumbe wote, ulimwengu huu ukawa uwanja wa vita ya ulimwengu, ambao kutokana nao Mungu wa upendo hatimaye atathibitika kuwa mwenye haki. Katika kuwasaidia watu wake katika pambano hili, Kristo anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuongoza, kulinda, na kutegemeza katika njia ya wokovu
Mafungu ya Biblia
Ufun. 12:4 – 9; Isaya 14: 12 – 14; Ezek. 28:12 – 18; Mwa. 3; Warumi 1:19 – 32; 5:12 – 21; 8:19 – 22; Mwa. 6 – 8; IIPet. 3:6l IWakor. 4:9; Webr. 1:14
