11. Kukua katika Kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha kuwa mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu hutupatia ushindi dhidi ya nguvu za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapotembea naye kwa imani, furaha, na uhakika wa upendo wake. Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu. Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na Mwokozi wetu tunawekwa huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya nguvu za uovu, ujinga, na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali. Katika uhuru huu mpya ndani ya Kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake, tukilitafakari neno lake na majaaliwa yake, tukiimba sifa zake, tukikusanyika pamoja kwa ajili ya ibada, a kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo wale wanaotuzunguka na katika kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia ya Roho hugeuza kila wasaa na kila kazi kuwa uzoefu wa kiroho
Mafungu ya Biblia
Zab. 1:1, 2; 23:4; 77:11, 12; Kol. 1:13, 14; 2:6, 14, 15; Luka 10:17 – 20; Efeso 5:19, 20; 6:12 – 18; IThes. 5:23; IIPet. 2:9; 3:18; IIWakor. 3:17, 18; Filipi 3:7 – 14; IThes, 5:16 – 18; Math. 20:25 – 28; Yoh. 20:21; Gal. 5:22 – 25; Warumi 8:38, 39; IYoh. 4:4; Waebr. 10:25.
