P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 24

Huduma ya Kristo katika Hekalu la Mbinguni

24. Huduma ya Kristo katika Hekalu la Mbinguni

Kuna hekalu mbinguni, hema la kweli lililosimamishwa na Bwana na siyo mwanadamu. Ndani yake Kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha kupatikana kwa ajili ya waumini fanaka za kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote. Alizinduliwa kuwa Kuhani wetu Mkuu na akaanza huduma yake ya uombezi wakati wa kupaa kwake mbinguni. Mnamo mwaka 1844, mwishoni mwa kipindi cha unabii wa siku 2300, aliingia katika awamu ya pili na ya mwisho ya huduma yake ya upatanisho. Ni kazi ya hukumu ya upelelezi ambayo ni sehemu ya mwisho ambayo hatimaye itakomesha dhambi yote, iliyokuwa mfano wa kutakaswa kwa hekalu la kale la Waebrania katika siku ya upatanisho. Katika huduma hiyo kielelezo hekalu lilitakaswa kwa damu ya wanyama wa kafara, lakini mambo ya mbinguni hutakaswa kwa kafara kamili ya damu ya Yesu. Hukumu ya upelelezi hufunua kwa viumbe wa mbinguni ni nani miongoni mwa wafu wamelala katika Kristo na hivyo, katika Yeye wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Pia inadhihirisha wazi ni nani miongoni mwa walio hai wanakaa ndani ya Kristo, wakishika amri za Mungu na imani ya Yesu, na katika Yeye, hivyo basi, wako tayari kwa ajili ya kuhamishwa kuingia katika ufalme wake wa milele. Hukumu hii huthibitisha haki ya Mungu katika kuwaokoa wale wanaomwamini Yesu. Hutangaza kwamba wale waliodumu kuwa watiifu kwa Mungu watapokea ufalme. Hitimisho la huduma hii ya Kristo itakuwa ndiyo mwisho wa kufungwa kwa mlango wa rehema ya wanadamu kabla ya marejeao ya Yesu

Mafungu ya Biblia

Waebr.8:1 – 5; 4:14 – 16; 9:11 – 28; 10:19 – 22; 1:3; 2:16, 17; Dan. 7:9 – 27; 8:13, 14; 9:24 – 27; Hes. 14:34; Ezek. 4:6; Walawi 16; Ufun. 14:6,7; 20:12; 14:12; 22:12