P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 14

Umoja katika Mwili wa Kristo

14. Umoja katika Mwili wa Kristo

Kanisa ni mwili mmoja ulio na washiriki wengi, walioitwa kutoka kila taifa, kabila, lugha, na watu. Katika Kristo tu viumbe wapya; ubainishi wa rangi, tamaduni, elimu, na taifa, na tofauti kati ya tabaka ya juu na ya chini, tajiri na masikini, mwanamume na mwanamke, havipaswi kuleta mgawanyiko miongoni mwetu. Sote tu sawa katika Kristo, ambaye kwa Roho mmoja ametufunga katika ushirika mmoja pamoja na yeye na sisi wenyewe kwa wenyewe; tunapaswa kutumika na kutumikiwa pasipo upendeleo au kusita. Kupitia kwa ufunuo wa Yesu Kristo katika Maandiko tunashiriki imani na tumaini moja,, na tunawafikia wote kwa ushuhuda mmoja. Umoja huu una chimbuko lake katika umoja wa Mungu mmoja mwenye nafsi tatu ambaye ametufanya sisi kuwa watoto wake

Mafungu ya Biblia

Warumi 12:4, 5; IWakor. 12:12 – 14; Math. 28:19, 20; Zab. 133:1; IIWakor. 5:16, 17; Mdo. 17:26, 27; Wag. 3:27, 29; Wakol. 3:10 – 15; Waef. 4:14 – 16; 4:1 – 6; Yoh.17:20 – 23