16. Meza ya Bwana
Meza ya Bwana ni ushirika katika mfano wa mwili na damu ya Yesu kama udhihirisho wa imani katika yeye, Bwana na Mwokozi wetu, katika uzoefu huu wa ushirika Kristo anakuwepo kukutana na kuwaimarisha watu wake. Kadiri tunavyoshiriki, kwa furaha tunatangaza mauti ya Bwana mpaka arudipo tena. Maandalizi kwa ajili ya Meza ya Bwana hujumuisha kujihoji nafsi, toba na ungamo. Bwana aliamuru huduma ya kutawadhana miguu kumaanisha kutakaswa upya, kuonyesha nia ya kutumikiana wenyewe kwa wenyewe katika unyenyekevu ufananao na wa Kristo, na kuungana mioyo yetu katika upendo. Huduma ya meza ya Bwana ni wazi kwa waumini wote Wakristo
Mafungu ya Biblia
IWakor. 10:16, 17; 11:23 – 30; Math. 26:17 – 30; Ufu. 3:20; Yoh. 6:48 – 63; 13:1 – 17
