17. Karama za Roho na Huduma
Mungu huwakirimia washirki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya upendo kwa ajili ya mema ya kawaida ya kanisa na ya wanadamu. Zikitolewa kwa wakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humgawia kila mshiriki kama apendavyo yeye, karama hizo hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa na kanisa katika kutekeleza shughuli zake zilizoamuriwa na Mungu. Kulingana na Maandiko, karama hizi hujumuisha huduma kama imani, uponyaji, unabii, mahubiri, mafundisho, utawala, upatanisho, huruma, na huduma ya kujinyima na ufadhili kwa ajili ya msaada na faraja kwa watu. Baadhi ya washiriki huitwa na Mungu na kukirimiwa na Roho kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji, uinjilisti, utume, na huduma za kufundisha zinazohitajika hasa katika kuwapatia zana washiriki kwa ajili ya huduma, kulijenga kanisa hadi ukomavu wa kiroho, na kukuza umoja wa imani na maarifa ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia karama hizi za kiroho kama mawakili waaminifu wa neema mbali mbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi ya mivuto miharibifu ya mafundisho ya uongo, na hukua kwa ukuaji unaotoka kwa Mungu, na hujengeka imara katika imani na upendo
Mafungu ya Biblia
Warumi 12:4 – 8; IWakor. 12:9 – 11, 27, 28; Waef. 4:8, 11 – 16; Mdo 6:1 – 7; ITim. 3:1 – 13; IPet. 4:10, 11.
