P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 19

Sheria ya Mungu

19. Sheria ya Mungu

Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimetiwa pamoja katika amri kumi na mfano wake ulidhihirishwa katika maisha ya Kristo. Nazo zinadhihirisha upendo wa Mungu, mapenzi yake, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano nazo ni sharti kwa watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ndiyo msingi wa agano la Mungu na watu wake na kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia uwakala wa Roho Mtakatifu zinasonda dhambi na kuamsha hisia za hitaji la Mwokozi. Wokovu wote ni katika neema, na si kwa matendo, lakini tunda lake ni utii kwa amri kumi. Utii huu hukuza upendo wetu kwa Bwana na wajibu kwa ajili ya wanadamu wenzetu. Utii wa imani hudhihirisha uwezo wa Kristo kubadilisha maisha na hivyo huimarisha ushuhuda wa Kikristo

Mafungu ya Biblia

Kut. 20:1 – 17; Zab. 40:7, 8; Math. 22:36 – 40; Kumb. 28:1 – 14; Math. 5:17 – 20; Waebr. 8:8 – 10; Yoh. 15:7 – 10; Waef. 2:8 – 10; IYoh. 5:3; Warumi 8:3, 4; Zab. 19:7 – 14