27. Milenia (miaka elfu) na mwisho wa dhambi
Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa Kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati ya ufufuo wa kwanza na wa pili. Wakati huo waovu waliokufa watahukumiwa; dunia itakuwa ukiwa na utupu bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na shetani na malaika zake. Mwishowe Kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu watashuka duniani kutoka mbinguni. Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao pamoja na shetani na malaika zake watauzingira mji; lakini moto kutoka kwa Mungu utawateketeza na kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi milele
Mafungu ya Biblia
Ufun. 20; IWakor. 6:2, 3; Yer. 4:23 – 26; Ufun. 21:1 – 5; Malaki 4:1; Ezek. 28:18, 19
