P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 10

Uzoefu na Wokovu

10. Uzoefu na Wokovu

Katika upendo usio na mwisho na rehema zake Mungu alimfanya Kristo, asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwamba katika yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu. Tukiongozwa na Roho Mtakatifu tunatambua hitaji letu, tunakiri hali yetu ya kuwa wenye dhambi, tunatubu maasi yetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana Kristo, kama Mbadala na Kielelezo. Imani hii inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo wa kimbimgu wa Neno na ni karama ya neema ya Mungu. Kupitia kwa Kristo tunahesabiwa haki, tunafanywa kuwa wana na binti za Mungu, na kukombolewa kutoka katika hali ya kuwa chini ya dhambi. Kupitia kwa Roho tunazaliwa upya na kutakaswa; Roho hufanya upya nia zetu, huandika sheria ya Mungu ya upendo katika mioyo yetu, na tunapewa uwezo wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani yake tunakuwa washirika wa asili ya uungu na tuna hakika ya wokovu sasa na katika hukumu

Mafungu ya Biblia

IIWakor. 5:17 – 21; Yoh. 3:16; Wag. 1:4; 4:4 – 7; Tito 3:3 – 7; Yoh. 16:8; Wag. 3:13, 14; IPet. 2:21, 22; Warumi 10:17; Luka 17:5; Marko 9:23, 24; Waef. 2:5 – 10; Warumi 3:21 – 26; Wakol. 1:13, 14; Warumi 8:14 – 17; Wag. 3:26; Yoh. 3:3 – 8; IIPet. 1:3, 4; Warumi 8:1 – 4; 5:6 – 10