12. Kanisa
Kanisa ni jamii ya waumini wanaimkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao. Katika kufungamana na watu wa Mungu katika nyakati za Agano la kale, tunaitwa kutoka katika ulimwengu; na tunajiunga pamoja kwa ajili ya huduma kwa wanadamu wote, na kwa ajili ya tangazo la injili ulimwenguni mwote. Kanisa linapata mamlaka yake kutoka kwa Kristo, aliye Neno lililofanyika mwili, na kutoka katika Maandiko, ambayo ndiyo Neno lililoandikwa. Kanisa ni jamaa ya Mungu; waliofanywa na Yeye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi katika msingi wa agano jipya. Kanisa ni mwili wa Kristo, jamii ya wale wenye imani ambayo Kristo mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa ili apate kulitakasa na kulisafisha. Wakati wa kurudi kwake kwa ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewe kanisa lenye utukufu, waaminifu wa karne zote, walionunuliwa kwa damu yake, lisilo na waa au kunyanzi, lakini takatifu na lisilo na ila
Mafungu ya Biblia
Mwa. 12:3; Mtdo. 7:38; Waef. 4:11 – 15; 3:8 – 11; Math. 28:19, 20; 16:13 – 20; 18:18; Waef. 2:19 – 22; 1:22, 23; 5:23 – 27 Wakol. 1:17, 18
