P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 21

Uwakili

21. Uwakili

Sisi tu mawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa na yeye wakati na fursa, uwezo, na mali, na mibaraka ya dunia na rasilimali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake sahihi. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya uaminifu kwake na kwa wandadmu wenzetu, na kwa kurudisha zaka na kutoa sadaka kwa ajili ya utangazaji wa injili Yake na kwa utengemezaji na ukuaji wa kanisa lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya malezi katika upendo na ushindi dhidi ya choyo na tamaa. Wakili hufurahia mibaraka inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake

Mafungu ya Biblia

Mwa. 1:26 – 28; 2:15; INyak 29:14; Hagai 1:3 – 11; Malaki 3:8 – 12; IWakor. 9:9 – 14; Math.23:23; IIWakor. 8:1 – 15; Warumi 15:26, 27